WANAUME WAJENGEWA UWEZO KUTOKOMEZA MILA, DESTURI KANDAMIZI

Photos: 

Shirika la Agape mkoani Shinyanga ambalo linafanya shughuli mbalimbali za kijamii , limetoa elimu ya kuwajengea uwezo wanaume wilayani Kishapu mkoani hapa, namna ya kupambana kutokomeza Mila na Desturi Kandamizi, ambazo zimekuwa kichocheo kikubwa cha kushamili Mimba na Ndoa za utotoni.

Shirika hilo linatekeleza mradi wake wa kutokomeza Mila na Desturi Kandamizi wilayani Kishapu kwa muda wa miaka miwili, kuanzia (2017-2019) kwa ufadhili wa Shirika la Save The Children, ambapo mradi huo unatekelezwa kwenye Kata 12 wilayani humo, kwa lengo la kumaliza matukio ya Mimba na Ndoa za utotoni.

Elimu hiyo ya kuwajengea uwezo wanaume hao imefanyika Februari 26 mwaka huu Katika Kata ya Ukenyenge wilayani Kishapu, na kukutanisha baadhi ya wanaume kutoka Kata za Ngofila, Talaga, Itilima, Kiloleli, Lagana, na Mwamashela, ambapo kesho watatoa elimu hiyo hiyo katika Kata za Somagedi, Bunambiu, Mwamalasa, Shangihilu, Masaga na Mwakiponya.