+255 746 237 265

info@tanlap.or.tz

KONGAMANO LA HUDUMA ZA MSAADA WA KISHERIA MWAKA 2023

TANLAP imepata nafasi ya kushiriki katika kongamano la huduma za msaada wa kisheria mwaka 2023 lililoandaliwa na Wizara ya Katiba na Sheria na kufanyika jijini Arusha. Kongamano hilo limefanyika tarehe 17 na 18 Agosti,2023. Mkurugenzi Mtendaji wa TANLAP Bi. Christina Kamili alipata nafasi ya kuzungumzia mchango wa mashirika kwenye ustawi wa mashirika ya watoa msaada wa kisheria na kuimarika kwa upatikanaji wa haki.
Kauli mbiu katika kongamano hilo ni "Msaada wa Kisheria kwa Haki, Usawa, Amani na Maendeleo"
#haki #amani #usawa #maendeleo