+255 746 237 265

info@tanlap.or.tz

MAFUNZO KWA WASAIDIZI WA KISHERIA KUHUSU MASUALA MBALIMBALI YAHUSUYO UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA

Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano kutoka TAMISEMI Bi. Nteghejwa Hosseah amewataka wasaidizi wa kisheria katika wilaya zote nchini, kwenda kutoa elimu sahihi ya masuala ya uchaguzi kwa wapiga kura.

Amesema haya leo wakati akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo kwa wasaidizi hao yaliyofanyika katika ukumbi wa hotel ya African Dream mkoani Dodoma.

Aidha, amesisitiza kujiepusha na migogoro isiyo ya lazima kwa wagombea na wapiga kura na kuongeza kuwa maafisa wasaidizi wa sheria kutoa elimu hiyo ya uchaguzi kwa umakini na weledi mkubwa.

Mafunzo hayo kwa wasaidizi wa kisheria yameandaliwa na TANLAP, ambao wamepewa kibali cha kuwa mwangalizi wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa nchi nzima kwa ufadhili wa USAID Tanzania kupitia mradi wa Wananchi Tuamue (Let's Decide).

#WananchiTuamue